Mtandao wa Instagram ni mmoja ya mitandao inayo ongeza kwa kutumiwa na watu wengi hasa hapa Tanzania.

Hii imefanya watu wengi kuwa na akaunti kupitia mtandao huo na kusababisha kuwa vigumu kupata username bora ambayo unaweza kutumia kwenye akaunti yako.

enter image description here

Ni wazi wote tunajua umuhimu wa kuwa na username yenye jina lako, au jina la biashara yako. Sasa kama kwa namna yoyote umeona kama username yako imechukuliwa unaweza kutumia njia hii kupata username bora yenye kufanana na jina lako au brand yako.

Tengeneza Username Instagram

Kwa kuanza ni vizuri ufahamu kuwa njia hii itakusaidia kama unalo jina tayari, na pia kama bado huna jina. Kwa awamu ya kwanza twende tuka angalie ukiwa na jina.

Kwa kuanza tembelea tovuti ya namechk.com, kisha baada ya hapo andika jina unalotaka kwenye sehemu ya kutafuta.

enter image description here

Baada ya kundika jina moja kwa moja bofya kitufe cha search na utaweza kuona kama jina hilo linapatikana kwenye mitandao ya kijamii kama instagram na mingine au kama limesha chukuliwa.

Pia utaweza kuona domain ya jina lako kama imesha chukuliwa au pia kama haija chukuliwa pia utaweza kuona.


Sasa kama kwa namna yoyote huna wazo la username unayotaka kutumia kwenye mtandao hasa Instagram unaweza kutumia tovuti nyingine ya businessnamegenerator.com

enter image description here

Unaweza kutembelea tovuti hiyo hapo juu kisha andika neno moja linalo husu biashara yako na moja kwa moja bofya sehemu ya Kusearch.

Baada ya hapo utaweza kuona majina mbalimbali ambayo unaweza kutumia kulingana na aina ya biashara unayotaka kumili. Baada ya hapo kuhakikisha kuwa username utakayo ipata haitumiwi na mtu mwingine unaweza kurudi kwenye tovuti ya kwanza kuangalia kama username uliyo itengeneza kama inapatikana na haitumiwi na mtu mwingine.

Kwa kufanya hivyo bila shaka utakuwa umepata username ya kutumia kwenye mtandao wa Instagram.

Kumbuka pia hakikisha unachukua username yako haraka kabla haicha chukuliwa na mtu mwingine kupitia tovuti ya kwenye bio.

Unaweza kupata link ambayo ina fanana kabisa na username yako hivyo harakisha na tengeneza username yako sasa uweze kupata link ya kwenye.bio inayo fanana na username yako.

Tengeneza Link ya Kwenye.Bio Hapa

Kuwa na akaunti ya kwenye bio ni bure kabisa na unaweza kutengeneza akaunti yako kwa kubofya hapo juu na hutolipia kitu chochote.