Tiktok ni moja ya mtandao maarufu kwa sasa, mtandao huu kwa sasa una zaidi ya watumiaji Milioni 689 hadi mwezi wa January mwaka huu 2021.
Kutokana na mtandao wa Tiktok kutumiwa na watu wengi zaidi ni wazi kuwa kila mtumiaji anatakiwa kuwa kwenye mtandao huu. Kama bado huja download app ya Tiktok, basi huu ni muda sahihi wa kufanya hivyo.
Kupitia makala ya leo nitaenda kuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kuweka link kwenye bio yako moja kwa moja kwenye mtandao wa Tiktok. Njia hii ni rahisi na unaweza kufanya moja kwa moja kwenye simu yako.
Weka Link Kwenye Bio TikTok
Kwa kuanza unatakiwa kupakua app ya Tiktok, kisha tengeneza profile. Kumbuka hutoweza kuweka link kwenye bio yako hadi utakapo badilisha ukurasa wako kuwa ukurasa wa kibiashara.
Unaweza kubadilisha profile yako ya Tiktok kuwa ya kibiashara kwa kufuata maelezo yafuatayo marahisi.
Baada ya kutengeneza kurasa yako moja kwa moja bofya kwenye profile yako kisha vitufe vitatu vya menu vilivyopo juu upande wa kulia.
Baada ya hapo moja kwa moja utaona Settings mbalimbali na chagua sehemu ya Manage account ambayo ni ya kwanza kabisa.
Baada ya hapo moja kwa moja bofya sehemu ya Switch to Business Account. Baada ya hapo bofya Next kuendelea kufuata maelekezo na kukamilisha kubadilisha profile yako ya Tiktok kuwa ya kibiashara.
Baada ya kuchagua Category na kufanya setup ya ukurasa wako moja kwa moja hatua ya mwisho bofya Edit Profile.
Baada ya kubofya hapo sasa unaweza kuendelea kwa kuweka link kwenye bio kwa kupitia sehemu ya Bio kama unavyoweza kuona hapo chini.
Baada ya hapo moja kwa moja unaweza kuendelea kwa kutengeneza bio yako kupitia hapa, unaweza kutengeneza bio yenye mitandao yako ya kijamii, biashara au hata kitu chochote ambacho unataka kuonyesha watu.
Haijalishi wewe unafanya biashara au hufanyi biashara unaweza kutengeneza bio yako kwani ni bure kabisa.
Kwa kufuata hatua hizi utakuwa umeweza kutengeneza bio link yako moja kwa moja kwenye mtandao wako wa Tiktok.