Kama wewe ni mmoja wa watu wenye kuhitaji kufanya (Sponsored) au kutangaza biashara Instagram basi njia hii itakusaidia sana.
Huna haja ya kuwa na akaunti ya benki bali unacho hitaji ni laini yako ya Vodacom Tanzania yenye huduma ya M-Pesa.
Kupitia njia hii utaweza kutangaza biashara yako kwa urahisi kupitia mtandao wa Instagram, gharama za matangazo zinaweza kuanzia Tsh 5000 ambayo unaweza kulipia kupitia huduma ya M-Pesa.
Ni muhimu kufuata vigezo na masharti ya matangazo kwani kila tangazo lazima lipitia kwenye idara ya ukaguzi ili kuhakikisha kama limefuata vigezo na masharti.
Unapoweka Tangazo lako subiri kwa muda ili tangazo lako likaguliwe. Kama Tangazo lako limekithi vigezo utatumiwa meseji kama halijakithi pia utahabarishwa.
Kujua zaidi Soma hapa