Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa mitandao ya kijamii ni wazi kuwa unafagamu kuhusu hashtag. Kama ufahamu kuhusu hashtag basi unasoma makala sahihi.

enter image description here

Kupitia makala hii nitaenda kukuelekeza jinsi ya kutumia hashtag, ikiwa pamoja na jinsi ya kupata hashtag bora ambazo unaweza kutumia kwenye mitandao yako ya kijamii.

Hashtag ni nini

Kwa kuanza unaweza ukawa unajiuliza hashtag ni nini.? Kama ulikuwa ufahamu hashtag ni alama ya # au "alama ya reli" "hash" ambayo hutumika kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuunganisha post yako na kwenye mda mbalimbali.

Kifupi kabisa unaweza kutumia hashtag kuweza kuunganisha post yako na mada maalum kwenye mitandao ya kijamii.

Hashtag ya kwanza ilianza kutumika hapo mwaka 2007 na ilitumiwa na Chris Messina kwenye mtandao wa Twitter na hiyo hapo chini ndio Tweet yenyewe.

enter image description here

Sasa baada ya kufahamu kidogo kuhsu Hashtag, sasa moja kwa moja twende nikuonyeshe jinsi ya kutumia Hashtag kukuza akaunti zako za mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kutumia Hashtag

Kama unataka kupata followers wengi au kukuza akaunti yako ya mitandao ya kijamii hasa twitter pamoja na Instagram basi ni muhimu sana kuzingatia masharti ya kutumia Hashtag.

Kwa kuanza ni muhimu kutumia hashtag zaidi kwenye mitandao ya Twitter na Instagram, njia hii inaweza kufanya kazi kwenye mitandao yote ila kupitia mfano huu tutatumia Instagram.

Unacho takiwa kufanya ni kupakua app hapo chini inayoitwa Hashtag Generator.

App hii ni tofauti kabisa na app nyingine ambazo umewahi kuzisikia. App hii inatumia mfumo maalum wa AI kuweza kujua ni aina gani ya hashtag ambazo unatakiwa kutumia kwenye picha au video ili kufikia watu wengi zaidi.

Unaweza kupata app hii kupitia hapa.

Baada ya kupakua app hii sasa endelea kwa kufungua app hiyo kisha endelea kwa kuchagua maneno, au picha au link ya post ili kupata hashtag.

Sehemu bora ni sehemu ya Photo, bofya hapo na kisha bofya "New Photo" alafu chagua picha ambayo unataka kupost kwenye akaunti yako ya Instagram alafu subiri baada ya muda app hiyo itakwambia ni hashtag gani ambazo ni bora kutumia kwenye picha hiyo.

enter image description here

Baada ya hapo kupata matokeo mazuri, copy hashtag ambazo zinatokea kwenye sehemu ya medium, sehemu ya Easy na kwenye sehemu ya hard copy hashtag moja tu.

enter image description here

Hii ni kwa sababu hashtag za hard ni ngumu kufikia watu wengi kutokana na kutumiwa na watu wengi sana na hashtag nyingine ni rahisi kwani hazitumiwi na watumiaji wengi.

Baada ya hapo tumia hashtag hizi kwenye mitandao yako ya kijamii kama instagram na mitandao mingine na utaweza kuona matokeo mazuri sana.

Mengine Muhimu

Ubora wa njia hii ni kuwa unaweza kutumia njia hii kwenye akaunti yako moja kama Instagram na baadae kutumia Instagram kupata followers kwenye akaunti yako ya Twitter.

Jinsi ya kufanya ni rahisi sana, unatakiwa kutengeneza link kwenye bio, Kisha kupitia link kwenye bio yako utaweza kuvutia wafuasi wako kukufuata kwenye mitandao yako mingine kama twitter, facebook na mitandao mingine.

Pia unaweza kuonyesha kazi zako moja kwa moja au unaweza kuuza bidhaa moja kwa moja kupitia link kwenye bio. Unaweza kutengeneza link yako bure kabisa kwa kubofya hapo chini.

Tengeneza link kwenye bio hapa Bofya hapa sasa kutengeneza

Kwa kufuata njia hizi na uhakika utaweza kukuza akaunti yako ya instagram kwa urahisi na kuweza kuvutia wateja kwenye akaunti zako nyingine kwa kutumia link kwenye bio.