Nadhani hadi sasa unajua kuwa Instagram ni moja ya mtandao ambao unatumiwa sana na wafanya biashara, kama wewe ni mmoja wa wafanyabiashara na unataka kutrend kwa urahisi Instagram basi unasoma makala sahihi.

enter image description here

Kupitia makala hii nitakwambia njia rahisi ya kusaidia kuweza kutrend kwa haraka na urahisi kupitia Instagram, hii ni pamoja na jinsi ya kufikia kwenye page ya Explore.

Kama ulikuwa hujui kuhusu page ya Explore kwenye mtandao wa Instagram basi endelea kusoma makala hii hadi mwisho.

Explore Page Instagram

Kama ulikuwa hujui Explore kwenye mtandao wa Instagram hii ni sehemu ambayo inaonyesha post mbalimbali kwa mtindo wa mtiririko wa post zinazo trend zaidi kulingana na mahali ulipo.

enter image description here

Ili kufikia ukurasa huu post zako unazopost kwenye akaunti yako ya Instagram zinatakiwa kuwa na sifa kadhaa, baadhi ya sifa hizo ni kama zifuatazo.

Sahau Kuhusu Likes

Kama unataka kufikia watu wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram basi kwa sasa sahau kuhusu likes. Kwa mujibu wa tovuti ya Instagram, Kupata likes nyingi hakusaidii post zako kufikia kwenye ukurasa wa Explore na hivyo huwezi kutrend kwa kupata likes zaidi bali...

Kupata Save nyingi ndio kuna saidia kufika kwenye page ya Explore na hivyo kutrend kwa urahisi. Hapa napo sema Save ni kile kitendo cha mtu kubofya kitufe cha Save kwaajili ya kuhifadhi post yako kwa ajili ya kusoma au kuangalia post yako baadae.

enter image description here

Unatakiwa kutengeneza post nzuri yenye maelezo ambayo unajua mteja wako au follower atahitaji kuyapitia kila siku au kila anapo hitaji.

Unaweza kutengeneza post ya maelezo ya muhimu ambayo unajua yatasaidia watumiaji wako na kupost kwenye post ya Slide ambayo huwa na post zaidi ya moja.

Hii ni muhimu kwa kuwa sehemu ya Explore huonyesha post ambazo hupata Engagement zaidi, kwa kupata Save nyingi hii inaonyesha post yako ni bora na ina engagement zaidi.

Hivyo basi kama unataka kutrend zaidi Instagram ikiwa pamoja na kupata likes nyingi zaidi, followers na kukuza biashara yako zaidi hakikisha una tengeneza post ambazo zitapata Save nyingi zaidi.

Hii haina maana kuwa likes na comment hazina maana bali zote kwa ujumla zikichangaywa zina weza kusaidia zaidi.