Baada ya kutengeneza akaunti, moja kwa moja hatua inayofuata ni kutengeneza link. Kutengeneza link ni rahisi hivyo unaweza kufutisha hatua hizi rahisi moja kwa moja.

Jinsi ya Kutengeneza Link

Baada ya kutengeneza akaunti na kuingia moja kwa moja utapelekwa kwenye dashboard, kwenye ukurasa huo shuka chini kidogo utaweza kuona sehemu iliyo andikwa Create link. Bofya hapo na utaona sehemu nyingine mbili zimefunguka yaani Biolink page na Shortened URL.

enter image description here

Biolink page

Kama unataka kutengeneza link ambayo unaweza kuweka vitu mbalimbali kama vile kuwa picha mbalimbali, link kwenda kwenye tovuti yako aukwenye mtandao mingine ya kijamii basi hakikisha unachagua Biolink page.

Bio link page inaweza kuwa mfano kwenye.bio/tanzaniatech au inaweza kuwa kwenye.bio/tanzaniatech zote link hizi zitakupeleka kwenye page yako unayotaka. Kumbuka unaruhusiwa kutengeneza link ya kwenye.bio/... lakini unaweza kutumia kwenye.bio/... kwenye mitandao yako ya kijamii.

Unaweza kuangalia mfano wa Biolink page kwa kutembelea biolink ya Tanzania Tech hapa, au unaweza kuangalia picha hapo chini. Unaweza kufanya mambo mengi sana kwa kutumia biolink yako tutaenda kuangalia hayo kwenye makala zinazofuatia.

enter image description here

Shortened URL

Shortened URL hii ni tofauti na Biolink page kwani kwa kutumia shortened URL utaweza kutengeneza link ambayo inawapeleka watumiaji moja kwa moja kwenye ukurasa fulani wa tovuti unayotaka.

Hii inaweza kuwa mitandao ya kijamii au mitandao mingine kama tovuti yako na vitu vingine mbalimbali.

Kupitia ukurasa makala hii bila shaka moja kwa moja utakuwa umeweza kutengeneza Biolink page pamoja na Shortened URL kwa urahisi na haraka.

Makala inayofuata nitaenda kuonyesha jinsi unavyoweza kuediti Biolink page yako pamoja na Shortened URL.